Kwenye Ukingo wa Thim

Tamthilia hii inaonyesha mambo mengi ya umuhimu kuhusu makabila ya Afrika ya Mashariki—kweli, sehemu zingine za Afrika pia.  Ni tamthilia iliyoandikwa kwa Kiswahili, kuhusu Mgikuyu na Mluo.  Nilisoma pahali pengine, juu ya website ya Oxford Journals, kwamba Kwenye Ukingo wa Thim inaonyesha ushindi wa Kiswahili kama lugha ya mataifa— yaani lugha ya dunia— ambayo inaweza kueleza hali ya Wagikuyu na Waluo kutumia lugha ya Kiswahili.  Lakini pia, makala hii inasema, tamthilia ni uungamaji wa kisirani cha ndoto ya mchanganyiko wa makabila wa Kenya kuishi pamoja kwa furaha katika nchi nzima—ndoto ya Ibrahim Hussein, lakini pia ndoto ya Ngugi wa Thiong’o.

Nafikiri shida za makabila ni kubwa sana.  Lakini sijui kama Kwenye Ukingo wa Thim ni uungamaji kama huo, kama makala inavyosema.  Shida za makabila ya Afrika zinatesa moyo wangu kabisa, kwa sababu ningetaka kuwaona watu wa dunia kuishi kwa furaha na amani.  Pengine hii ni ndoto yangu.  Lakini kwangu nafikiri inawezekana.  Si lazima kupotea umuhimu wa makabila.  Mtu anaweza kusherekea utamaduni na kabila zake, lakini bila kupigana na watu wa kabila nyingine.

Kwa hivyo sasa tunaweza kuona manufaa ya jasho la Watanzania kujenga umoja, kama tulivyoona katika masomo ya Vita vya Maji Maji.  Nimesema kwamba kuonyesha Watanzania kama walikuwa nchi nzima kabla ya ukoloni si kweli kabisa, na kuonyesha hivi kulikuwa na nia kwake.  Kinjeketile na Kumbukumbu za Vita vya Maji Maji zote mbili zilijaribu kuonyesha hivi.  Lakini si lazima kuamua kwamba hivi ni vibaya.  Nia kwake kulikuwa kujenga nchi ya umoja na nguvu ili ifanye kazi vizuri baada ya uhuru.  Sina elimu nyingi kuhusu makabila ya Tanzania na wakipigana mara nyingi leo.  Lakini inaonekana kwamba Tanzania ina shida chache kuliko Kenya, nchi ambayo hadithi ya Kwenye Ukingo wa Thim ni kuhusu.

Tunaweza kuona shida hizi hata leo, wakati wa uchaguzi wa Kenya mwaka wa 2007.  Inaonekana pia kwamba kuna shida nyingi za ufisadi kwenye Kenya kuliko Tanzania—sijui kama ni kweli kabisa, lakini.  Vilevile katika tamthilia ya Kwenye Ukingo wa Thim, kuna mambo ya kuishi katika zote mbili hali ya maisha ya kisasa na hali ya kukumbuka utamaduni na kabila.  Na siyo shida ya Wakenya tu—lakini pia wanafunzi na wafanyakazi kutoka nchi zingine.  Jambo muhimu leo ni jambo la maendeleo.  Kweli, Ben mwenye ukurasa wa 11 katika tamthilia alisema, “Mimi sizungumzii ukabila.  Nazungumzia maendeleo.  Maendeleo hasa, halisi.”

Sehemu hii ina miuktadha yake, mnamo 1988, wakati wa “structural adjustment.”  Lakini mpaka leo, ni swali la ngumu.  Mara nyingi sana maana ya maendeleo ni kuacha mila na desturi.  Nafikiri hii ni shida kubwa ya mashirika kama Benki ya Dunia—wanafikiri kwamba makabila ni kinyume cha maendeleo kabisa, na wengi hawaelewi mambo haya vizuri.  Si lazima kuacha mila na desturi.  Pia, nafikiri kuna shida kutumia neno la “maendeleo.”  Kutumia neno hili ni kama kusema nchi tajiri ni bora na zenye tabia njema kuliko nchi maskini, kwamba nchi maskini zinahitaji kuendelea kuwa kama nchi tajiri.  Nafikiri neno tofauti lingekuwa bora kutumia.

Tena shida za makabila.  Si lazima kuonyesha kabila kama ni kinyume cha “maendeleo,” ama kinyume cha kisasa.  Mila na desturi zimebadilisha zamani, na kuendelea kubadilisha mpaka leo—si sawa kama zamani sana.  Kwa hivyo, Afrika ya kisasa imeshaendelea.  Basi, kama imeendelea vizuri au vibaya lingekuwa swali.  Tunajua, kwa mfano, kwamba ufisadi ni shida.  Nafikiri baada ya kubadilishia njia za kufikri kwa wanafunzi na wafanyakazi wa maendeleo, shida nyingi zingewezekana kuboresha.

Najua dhana ya “maendeleo” ni kuboresha nchi, kuacha ufisadi, na kuzisaidia nchi kupata pesa zaidi.  Ina nia ya kuboresha maisha za watu.  Lakini haiwezi kufanya hivi kama inaendelea kutofahamu mambo ya makabila, na mila na desturi zao.  Na haiwezi kufanya hivi kama inaendelea kuwafikiria Waafrika kama wao ni chini kidatoni kwa ngazi ya maendeleo, ama wao ni hatua nyingi nyuma ya Ulaya na Amerika.

About Carol Jean Gallo

PhD student at Cambridge. Interested in local context and global affairs and the crossroads and misinterpretations between them.
This entry was posted in Insha za Kiswahili. Bookmark the permalink.

8 Responses to Kwenye Ukingo wa Thim

 1. joelson says:

  hongera Sana

 2. Aimable MUNEZERO says:

  kazi nzuri

 3. Aimable MUNEZERO says:

  Kazi nzuri sana mno. Endelea hivyo.

 4. Mpaji Joseph says:

  Safi, kazi nzuri!

 5. Mpaji Joseph says:

  Inapendeza kupata msaada wa mada zilizochangunuliwa vema mtandaoni!

 6. Mtanda says:

  Safi sana dada, Carol:) Nimeipenda blogu…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s