Zilizala

Zilizala: Maoni Kuhusu Tamthilia

Kwangu nafikiri tamthilia ya Zilizala ni muhimu sana.  Inaonyesha mambo mengi ya kisasa, hasa shida, kwenye Afrika ya Mashariki, kama ufisadi na kadhalika.  Lakini hii siyo sababu pekee inayoifanyia Zilizala ya muhimu.  Tamthilia hii vilevile ni kuhusu mambo mengine yenye maana kubwa.  Inataja mambo ya historia, mambo ya siasa, na mambo ya urafiki.  Pia tena, umuhimu wa tamthilia hii unaweza kuonwa na utumiaji wa lugha ya Kiswahili na utumiaji wa mada za fasihi.

Nilifikiri ilikuwa vizuri njia ya mwandishi amewaumba wahusika wenye tabia mbalimbali za kina.  Yaani, kila mhusika ana historia yake—hawakuzaliwa na hawaishi uvurunguni.  Kwa mfano, Udenda, Kumba, na Angela walijuana zamani walipokuwa marafiki.  Uhusiano huu unamruhusu mwandishi kuonyesha mabadiliko yanayoweza kutokea baada ya miaka mingi.  Aidha, mwandishi ametumia uhusiano huu kuonyesha kwamba siasa ya kisasa, baada ya ukoloni katika serikali za Afrika, siyo rahisi kama kusema kuna ufisadi na watu wabaya wa serikali tu.  Bali historia ya wahusika hawa watatu inaonyesha kwamba Udenda, aliyekuwa na ufisadi katika tamthilia, alipokuwa kijana alikuwa na maoni tofauti kuhusu maisha na siasa.  Yaani akikua kuwa mzee zaidi na kufanya kazi mwenye serikalini, alianza kutambua ugumu wa maisha wanapojitunza wowote wenyewe binafsi tu.

Kwa hivyo ilionekana kama Udenda amepoteza sehemu ya moyo wake.   Tunaposoma, tunataka kujua kwa nini ama vipi hivi vimetokea.  Kwa nini Udenda haamini maoni ya ujana wake sasa?  Kwa vipi aliweza kusahau maana ya Mafukara wa Ulimwengu, kama Kumba alivyosema?  Nilifikiri sehemu ya huzuni nyingi ilikuwa karasa za mwanzo za Onyesho la Pili Kumba na Udenda wanapoongea ujana wao. Kumba anamkumbusha Udenda walikuwa marafiki, walipokuwa chuo kikuu Udenda aliongoza migomo, na Udenda na Angela walikuwa wapenzi pamoja, na kadhalika.  Alimwambia Udenda, “Mwenzangu, umebadilika.”

Lakini Udenda anacheka kwa dharau tu.  Kweli anasema maneno makali sana ya dharau na kupoteza moyo wa ujana wake.  Anasema hivi Kumba anavyosmea ni vitu vya ujana.  Anasema kwamba Kumba anaota ndoto, na kupiga kura hakungebadilisha chochote.  Anasikia kidogo tu kwa mkewe Angela siyo kama walipokuwa vijana; hampendi Angela kama alivyompenda zamani, na hivi vinampa Angela huzuni nyingi.  Kwa hivyo mwandishi anaonyesho mambo mawili pamoja: ufisadi siyo kitu cha rahisi, na urafiki na upenzi wa zamani.  Nafikiri kuonyesha vitu hivi ni muhimu sana—kutaja mambo ya mabadiliko ya wengi wa serikali baada ya uhuru—kumtaja mmoja tu, Kenyatta mwenyewe.  Kwangu nafikiri hivi vinaonyesha kwamba serikali ya ukoloni ilipoondoka Afrika, ilibakia serikali baya kwa nchi za Afrika—halafu, si vigumu kufahamu vipi ni rahisi kwa watu kama Udenda wanakua kuwa na ufisadi na kusahau “ndoto” za ujana wakati wa uhuru na hata kabla.

Pia onyesho lenye mazungumzo ya Udenda na Angela linaonyesho vitu kama hivi.  Ukarasa wa 19 Udenda anajaribu kueleza kwamba hapendi kufanya anavyofanya lakini ni madaraka yake.  Inaonekana pia kwamba baada ya Udenda akiondoka maoni yake ya ujana, halafu Angela na Kumba wamekuwa wasaliti, hata kama ilikuwa Udenda amebadilika, siyo marafiki yake!  Ndiyo, anamwita Angela msaliti ukarasa wa 23.  Na kumjibu Udenda, Angela anajaribu kumkumbusha, “Tulikuwa sote Udenda.  Tukitetea umma, tukikutana usiku kutafakari.  Tukawasoma Fanon, Cabral, Rodney, Samora, Malcolm X… Halafu ukavuka upande wa pili, kumhudumia shetani.”

Aidha, ningetaka kusema vichache kuhusu mambo ya lugha na fasihi katika tamthilia hii.  Mwanzo, ni rahisi kuona kwamba mwandishi anatumia msamiati wa uzuri na ugumu.  Hata kama ilikuwa vigumu kusoma na ilichukua muda mrefu kusoma, nilifurahi kuona maneno mengi kama haya kwa sababu kila lugha inahitaji msamiati wa upana.

Mwandishi vilevile ametumia mada za maisha na fasihi, na vitu kufanyia tamthilia kuwa ya kisanaa.  Kwa mfano, zilizala ya Udenda si zilizala pekee katika tamthilia.  Inaonekana kwa mimi kwamba nchi nzima insikia zilizala za mabadiliko baada ya uhuru na kutoka ukoloni.  Mada hii inaweza kukuonwa shairi la ukarasa wa 65:

“Watawala hawa waweza kuaminika

Wakati wananchi wanaposumbuka?

Watawala hawa waweza kaminika

Wakati nchi inapoporomoka?”

Na katika shairi hili tena kuna maneno kudhihiri mada hii—kama “kurushia,” “kulipulia,” “kugeuza,” “kupinda,” na “kuvuruga.”  Kuna mifano mingine pia, kama msichana Atieno anapolia anamwambia Mama shida yake.  Alisema alitetemeka, nafikiri kutetemeka kama zilizala.

Nafikiri pia onyesho la mchezo ndani ya mchezo linafanyia Zilizala ya kisanaa.  Hasa mwisho wa mchezo ndani ya mchezo, msichana na mvulana walipokuwa na mzozo juu ya sabuni, unahitaji kujiuliza maana ya onyesho hili ni nini?  Na bado sina hakika, lakini nimefikiri kuhusu maana ya sabuni kwenye Afrika wakati wa ukoloni.  Hasa kama tulikuwa na sahihi tuliposema darasani kwamba Robben Island ni pahali pa gereza.  Lakini sijaamua nafikiri maana ni nini.

Nilipenda tamthilia hii sana, hata hivyo ilikuwa na maneno mengi magumu.  Hadithi ni nzuri na muhimu, na nimefurahi kusoma kitu cha kisanaa cha Kiswahili.

About Carol Jean Gallo

PhD student at Cambridge. Interested in local context and global affairs and the crossroads and misinterpretations between them.
This entry was posted in Insha za Kiswahili. Bookmark the permalink.

2 Responses to Zilizala

  1. Makokha mathew says:

    Poa xana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s